Vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vimeigharimu Ukraine $564.9bn (£429.3bn) kufikia sasa katika uharibifu wa miundombinu, kupoteza ukuaji wa uchumi na mambo mengine, kulingana na waziri wa uchumi wa Ukraine.
Mapigano hayo yameharibu kilomita 8,000 (maili 4,970) za barabara na mita za mraba milioni 10 za makazi, Yulia Svyrydenko alisema katika chapisho la mtandao wa kijamii.
Urusi inaendelea kusema kuwa inaendesha “operesheni maalum ya kijeshi” nchini Ukraine kwa lengo la kuipokonya silaha nchi hiyo.
Ukraine na washirika wake wa Magharibi wamesema msimamo huo ni kisingizio cha uvamizi usio na msingi.