ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, February 7, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Vodacom Tanzania PLC yaungana na Eutelsat kueneza mtandao wenye kasi katika maeneo yasiyofikiwa nchini

I am Krantz by I am Krantz
Mar 16, 2022
in HABARI
0
Vodacom Tanzania PLC yaungana na Eutelsat kueneza mtandao wenye kasi katika maeneo yasiyofikiwa nchini
0
SHARES
129
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT


Makubaliano yataongeza kasi ya upatikanaji wa huduma za kidijitali katika mikoa ambayo haijafikiwa nchini
Huduma hii itapatikana kupitia satelaiti yenye kasi kubwa ya EUTELSAT KONNECT
Makubaliano haya yanafuatia mafanikio ya majaribio yaliyofanywa na Vodacom na Eutelsat kuonesha ufanisi wa teknolojia ya satelaiti

Dar es Salaam, 15 Machi 2022 – Vodacom Tanzania, kampuni inayoongoza katika huduma za kiteknolojia nchini imetangaza kutia saini mkataba na shirika la Eutelsat Communications ambao utawezesha kuunganisha huduma kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na mtandao wa kidjitali mikoani kupitia satelaiti yenye kasi kubwa ya Eutelsat KONNECT.
Huduma hii mpya itatoa fursa kwa wafanyabiashara binafsi na wa kimataifa, sekta ya utalii na hoteli ambapo mafanikio yameonekana katika majaribio yaliyofanikiwa kwa Vodacom Tanzania PLC kupanua wigo wa upatikanaji huduma na kuwafikia watumiaji ambao walikuwa hawajafikiwa awali. Huduma hizi zitatolewa na Vodacom huku vifaa vikiunganishwa na Konnect Africa.
Akizungumza wakati wa kutangaza mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Sitholizwe Mdlalose alisema, “Tunafuraha kubwa kujumuisha huduma zetu kwenye satelaiti hii, tukitumia uwezo wa satelaiti mpya kabisa ya EUTELSAT KONNECT ambayo itatuwezesha kutimiza dhamira yetu ya kufikisha huduma za mtandao katika maeneo yote nchini.”
Aliongeza kusema kuwa kwa kutumia KONNECT, Vodacom itapanua mtandao wake kufikia asilimia 100 ya eneo lote la Tanzania, yaani kuunganisha mikoa na wilaya zote na vijiji bila kujali umbali husika, “kwa huduma hii, tutaunganisha kila mtu, hii ni pamoja na maeneo ambayo hayajafikiwa hivi sasa, ikiwa na kasi ya hadi 100Mbps” alisema mkurugenzi huyo.
Huduma hii inaendana na dhamira ya Vodacom Tanzania kuboresha upatikanaji wa huduma za kidijitali zenye kasi kwa watu wengi zaidi nchini kwa kubuni njia mpya za kufikisha huduma kwa watumiaji wote.
Toka ianze kutoa huduma mwishoni mwa mwaka 2020 EUTELSAT KONNECT ni satelaiti mpya yenye kasi kubwa inayotoa huduma kwa kasi na viwango vinavyohitajika. Ina rasilimali kubwa inayowezesha utoaji huduma za kasi ikiwa na mtandao unaofikia karibu eneo lote la Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika, hii inawezesha moja kwa moja kwa watumiaji na wafanyabiashara kupata huduma ya intaneti yenye kasi zaidi.
Mojawapo ya mikakati ya Vodacom Tanzania Plc ni ushirikishwaji kwa wote katika kuondoa mgawanyiko kwenye upatikanaji wa huduma za kidijitali, hivyo ushirikiano huu una uzito mkubwa kwa Vodacom, kwani utatoa huduma kwa watu ambao hawajawahi kupata huduma za mtandao tangu tupate uhuru.
Akichangia kwenye makubaliano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Konnect Africa, Philippe Baudrier alisema, “Tuna furaha kubwa kushirikiana na Vodacom Tanzania, kampuni inayoongoza barani Afrika katika sekta ya mawasiliano, kwa kupanua wigo wa mtandao wake nchini Tanzania. Mkataba huu unaonyesha jinsi ambavyo uwezo mkubwa wa satelaiti ya EUTELSAT KONNECT unaweza kutimiza mahitaji makubwa kwa maeneo ya bara la Afrika ambayo hayajafikiwa au yenye huduma hafifu na ina ashiria mafanikio katika maendeleo ya usambazaji wa huduma baada ya makubaliano yetu nchini Nigeria, Afrika Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)”

RelatedPosts

HIZI HAPA JEZI MPYA ZA SIMBA ZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

HIZI HAPA JEZI MPYA ZA SIMBA ZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Feb 7, 2023

HAJI MANARA AIJIA JUU BODI YA LIGI KISA CLEAN SHEETS, SIMBA SC

Feb 7, 2023

DAYOO AFUNGUKA KWANINI ANASEMA “NAITWA MANGI…”

Feb 7, 2023
Load More
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

HIZI HAPA JEZI MPYA ZA SIMBA ZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
HABARI

HIZI HAPA JEZI MPYA ZA SIMBA ZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023
TANZANIA, UAE ZASAINI KUHIFADHI MAZINGIRA
HABARI

TANZANIA, UAE ZASAINI KUHIFADHI MAZINGIRA

by ALFRED MTEWELE
Feb 7, 2023
YANGA KWENDA TUNISIA LEO NA WACHEZAJI 25
HABARI

HAMTAMUONA KOCHA NABI AIRPORT – ALLY KAMWE

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023
YANGA KWENDA TUNISIA LEO NA WACHEZAJI 25
HABARI

YANGA KWENDA TUNISIA LEO NA WACHEZAJI 25

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023
QUEIROZ KOCHA MPYA QATAR
HABARI

QUEIROZ KOCHA MPYA QATAR

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023
ATSU APATIKANA AKIWA HAI KUTOKA KWENYE VIFUSI
HABARI

ATSU APATIKANA AKIWA HAI KUTOKA KWENYE VIFUSI

by Shabani Rapwi
Feb 7, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In