Wachezaji kadhaa wa timu ya taifa ya soka ya Ukraine, akiwemo Oleksandr Zinchenko wa Man City na nyota wa West Ham Andriy Yarmolenko wameungana kuwaambia mashabiki, wachezaji na makocha kupinga propaganda ya Urusi na kukomesha umwagaji damu unaoendelea tangu Urusi wavamie Ukraine.
Wachezaji hao wamejirekodi wakizungumza kwenye video ya pamoja ili kuwasilisha ujumbe wanaotumai utachangia katika kumaliza vita hiyo inayoendelea. Hii imekuja baada ya jioni ya jana shirikisho la soka barani ulaya UEFA pamoja na shirikisho la soka duniani FIFA kutangaza kuvifungia vilabu vyote vya Urusi kushiriki michuano yote iliyochini ya UEFA.
Na hivyo kuziondoa timu za RB Salzburg kwenye ligi ya mabingwa ulaya na Spartak Moscow katika ligi ya Uropa, pamoja na kuifungia timu ya taifa ya Urusi kushiriki michuano yote ya kimataifa chini ya FIFA ikiwemo kombe la Dunia hadi watakapo toa tamko lingine.
Mashambulio hayo mashariki mwa Ulaya sasa yameingia katika siku yake ya sita ya mapigano ya kikatili, huku maelfu ya watu wakihofiwa kuuawa huku majeshi ya Urusi yakijaribu kuuzingira mji mkuu wa Kyiv nchini Ukraine.