Zari The Bosslady ameweka bayana mambo kadhaa kuhusu mahusiano yake wa sasa na aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz.
Akizungumza katika show ya ‘Young, Famous and African’, Zari aliweka wazi kuwa kwa sasa hakuna mahusiano yoyote ya kimapenzi kati yake na Diamond.
“Mimi na Diamond hatujarudiana, huwa anakuja kunitembea kisha anaondoka, hatuko pamoja, hatushiriki tendo la ndoa, hata hatulali pamoja ama kugusana,” alisema Zari.
Mama huyo wa watoto watano alieleza kuwa Diamond humtembea nyumbani kwake mara kwa mara kwa ajili ya kuona watoto wao wawili, Tiffah na Nillan.
cc @zarithebosslady @diamondplatnumz