Mahakama ya Moscow, nchini Urusi imeamuru kukamatwa kwa mali na fedha za kampuni ya Google, zenye thamani ya USD Milioni 7, hii inatokana na kesi inayohusu vikwazo ambavyo kampuni ya teknolojia ya Marekani imeweka kwenye chaneli ya YouTube ya kampuni moja maarufu ya televisheni nchini humo.
–
Kampuni ya Alphabet Inc.’s ama Google haikujibu mara moja ombi la maoni, Mashirika ya habari ya Urusi yaliripoti kuwa kesi hiyo inahusu Televisheni ya GPM Entertainment ya Gazprom Media Holding, ambayo iliwasilisha kesi, ikiitaka Google kurejesha ufikiaji wa akaunti yake ya YouTube.
–
YouTube, ambayo imezuia vyombo vya habari vinavyofadhiliwa na Serikali ya Urusi duniani kote, iko chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa wadhibiti wa mawasiliano wa Urusi na wanasiasa.
–
Urusi imezuia makampuni mengine ya kigeni ya mtandao, ikiwa ni pamoja na Meta Platforms Inc.’s (FB.O) Facebook na Instagram, huku ikipambana kudhibiti mtiririko wa taarifa baada ya kutuma makumi ya maelfu ya wanajeshi nchini Ukraine Februari 24, 2022. YouTube bado inapatikana kwa sasa.