Watu wanne ambao ni askari wa Jeshi la Polisi wawili na mahabusu wawili wamefariki dunia, kwenye ajali iliyotokea katika kijiji cha Ibanda mkoani Geita.
–
Ajali hiyo imetokea April 27 majira ya saa 10:00 jioni ikihusisha gari la Polisi namba PT 3798 Toyota Landcruiser lililokuwa likitokea Geita kusikiliza kesi mahakamani, kugongana na Lori aina ya Scania namba T 691 DBQ mali ya kampuni ya Nyanza lililokuwa likitokea mkoani Mwanza kuelekea mkoani Geita.
–
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe ameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni gari la Polisi kupata hitilafu.
–
Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa mkoa wa Geita dokta Mfaume Salum anasema alipokea majeruhi watatu na wote wamepatiwa matibabu mmoja anaweza kuruhusiwa.