Mtandao wa YouTube umeifungia akaunti ya mwanamuziki @diamondplatnumz kwa kukiuka masharti na sheria za mtandao, ikiwa ni siku chache tu zimepita toka kudukuliwa.
ADVERTISEMENT
Kwa mujibu wa meneja wa msanii huyo, Babu Tale amesema akaunti hiyo imedukuliwa na hii ni mara ya pili inatokea hali kama hiyo.
YouTube ya Diamond imefutwa ikiwa na zaidi ya Subscribers milioni 6.5 na jumla ya watazamaji Bilioni 1.5. Ilikuwa na zaidi ya video 700.
ADVERTISEMENT