ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, May 22, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Al Barakah ya Benki ya CRDB yawagusa RC na Sheikh Mkuu Tanga

I am Krantz by I am Krantz
Apr 10, 2022
in BIASHARA
0
Al Barakah ya Benki ya CRDB yawagusa RC na Sheikh Mkuu Tanga
0
SHARES
43
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Mkuu wa Idara ya Hazina ya Benki ya CRDB, Bw. Alex Ngusaru akizungumza na wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga wakati wa futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.


RelatedPosts

Benki ya CRDB yaahidi neema kwa wafanyabiashara kati ya Tanzania na DRC

Benki ya CRDB yaahidi neema kwa wafanyabiashara kati ya Tanzania na DRC

May 11, 2022

BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO MBILI ZA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI KITAIFA DODOMA

Apr 29, 2022

Dkt. Tulia aipongeza Benki ya CRDB kuuenzi mwezi Ramadhani

Apr 20, 2022
Load More


ADVERTISEMENT

Wateja na wadau wa Benki ya CRDB  Mkoa wa Tanga wakishiriki futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.



Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa akizungumza na wateja na wadau wa Benki ya CRDB  Mkoa wa Tanga wakati wa futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.



Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa akishiriki futari na wateja na wadau wa Benki ya CRDB wa Mkoa wa Tanga.



Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Sheikh Juma Luwuchu akizungumza na wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga wakati wa futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.


Wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga waliojitokeza kushiriki futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.



Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa akiwa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya CRDB, Bi. Chiku Issa (wa pili kushoto) wakikabidhi vyakula kwa kituo cha wenye uhitaji cha Imani Chumbageni ikiwa ni sehemu ya mchango wa Benki ya CRDB kwa kituo hicho katika mfungo wa mwezi Ramadhani. 


Wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga waliojitokeza kushiriki futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.





Wateja na wadau wa Benki ya CRDB  Mkoa wa Tanga waliojitokeza kushiriki futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.



Wafanyakazi wanawake wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushiriki futari na wateja na wadau wa benki wa Mkoa wa Tanga.





 


Tanga 9 Aprili 2022 – Huduma ya Al Barakah ya Benki ya CRDB inayozingatia misingi ya kutotoza au kupokea riba imewafurahisha wananchi, wadu na viongozi wa mkoa wa Tanga. Hilo limebainika katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wateja, wadau na wenye uhitaji katika Mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Benki hiyo kufuturisha kipindi cha mfungo wa Ramadhani. Hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Sheikh Juma Luwuchu.

Akizungumza katika futari hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Hazina na Masoko ya Mitaji wa Benki ya CRDB, Bw. Alex Ngusaru alisema kuwa Benki ya CRDB imeendelea kusikiliza maoni ya wateja na kuendelea kuleta sokoni bidhaa na huduma bunifu zinazoendana na mahitaji ya soko.

“Uanzishwaji wa huduma ya Al Barakah unadhihirisha ni kwa kiasi gani ambavyo Benki yetu inaishi kauli mbiu yake ya “Benki Inayomsikiliza Mteja” kwani kupitia kusikiliza maoni ya wateja wetu ndipo tulipoweza kuja na huduma hii makhususi kwa ajili ya wenzetu ambao wanaamini katika misingi ya kutopokea wala kutozwa riba” alisema Ngusaru.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa ambae alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika hafla hiyo aliipongeza na kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa futari hiyo kwa wakazi wa Tanga pamoja na kuandaa vyakula kwa ajili ya wenye uhitaji ili kuwasaidia katika kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani. Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa ujio wa huduma ya Al Barakah utakua chachu ya kuongeza wigo kwa kufikisha huduma za fedha kwa Watanzania kwani wapo ambao walikua hawawezi kutumia huduma za benki kwa kuwa tu haziendani na misingi ya imani yao.

“Nawapongeza sana Benki ya CRDB kwa hili la futari na kugusa wenye uhitaji lakini zaidi niwapongeze kwa kuja na huduma hii makhusi ya Al Barakah ambayo inaendana na imani ya wenzetu wasioamini katika kutozwa au kupokea riba” alisema Mh. Mgandilwa.

Kwa upande wake Shekhe wa mkoa wa Tanga Juma Luwuchu ambae aliambatana na masheikh wengine wa Mkoa alitoa shukrani na pongezi kwa Benki ya CRDB kwa kuipa heshima Tanga kwa kuamua kuifanya kuwa moja kati ya mikoa ambayo benki itaandaa futari kwa mwaka huu lakini zaidi akifurahishwa na huduma ya Al Barakah inayofata misingi ya Sharia.

Sambamba na hilo Sheikh Luwuchu aliwaasa Waislamu pamoja na taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki ya CRDB cha kukumbuka wenye uhitaji katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan huku akiwataka Waislamu kuhakikisha wanadumisha yale mema na mazuri yaliyoelekezwa katika Quran tukufu.

“Benki ya CRDB wametuonyesha mfano mzuri kwa kuwakumbuka wateja na wadau wao lakini hawakuishia hapo wamekumbuka pia watoto wetu wenye uhitaji kutoka kituo cha Imani Chumbageni,” alisema Sheikh Luwuchu.

Kituo cha Imani Chumbageni ambao pamoja na kualikwa katika futari hiyo pia walikabidhiwa vyakula mbalimbali ikiwemo ngano, sukari, tambi, tende na mafuta ya kupikia ili kuwasaidia kupata futari kipindi cha mfungo wa mwezi Ramadhani.

Related

Tags: CRDB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA
BIASHARA

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO
BIASHARA

WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
BENKI YA EQUITY YAZINDUA  KAMPENI YA ‘ISHI KISASA PESA MZIGO’’
BIASHARA

BENKI YA EQUITY YAZINDUA KAMPENI YA ‘ISHI KISASA PESA MZIGO’’

by Ally Hamis Zingizi
May 18, 2022
TFS KANDA YA KUSINI KUTUMIA FILAMU YA ROYAL TOUR KUONGEZA WATALII KUSINI
BIASHARA

TFS KANDA YA KUSINI KUTUMIA FILAMU YA ROYAL TOUR KUONGEZA WATALII KUSINI

by Ally Hamis Zingizi
May 15, 2022
MIRADI YAKO IKO SALAMA UKIWA UMEBIMA NA BENKI YA NMB
BIASHARA

MIRADI YAKO IKO SALAMA UKIWA UMEBIMA NA BENKI YA NMB

by I am Krantz
May 14, 2022
TPA HOSTS LMC DELEGATION FOR BUSINESS TALKS
BIASHARA

TPA HOSTS LMC DELEGATION FOR BUSINESS TALKS

by I am Krantz
May 13, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In