ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Wednesday, March 22, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

AXIAN TELECOM PAMOJA NA ROSTAM AZIZI WAKAMILISHA MCHAKATO WA KUMILIKI KAMPUNI ZA MAWASILIANO ZA MILLICOM KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

I am Krantz by I am Krantz
Apr 6, 2022
in HABARI
0
AXIAN TELECOM PAMOJA NA ROSTAM AZIZI WAKAMILISHA MCHAKATO WA KUMILIKI KAMPUNI ZA MAWASILIANO ZA MILLICOM KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
0
SHARES
138
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

 

Muungano wa AXIAN Telecom na Rostam Aziz leo umetangaza kukamilika kwa mchakato wa umiliki wa kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania Public Limited Company (Tigo na Zantel) katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mchakato huu unaleta takribani wateja milioni 14 wa simu za mkononi kwa AXIAN Telecom na kuharakisha ukuaji wa kampuni hii barani Afrika ambapo kwa sasa imefika nchi nane katika bara hili.

RelatedPosts

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

Mar 21, 2023

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

Mar 21, 2023

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

Mar 21, 2023
Load More

Mpango kabambe wa ukuaji na wenye matumaini wa muungano wa AXIAN Telecom unajumuisha uwekezaji mkubwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo, ili kuimarisha ubora wa huduma zitolewazo na kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania PLC.
Kwa kununuliwa kwa MIC Tanzania PLC, AXIAN Telecom inafungua ukurasa mpya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunayo furaha kuanza safari hii ya kusisimua na wenzetu wa hapa (Tanzania) na ninaamini kwa pamoja tutafanikisha mambo makubwa yatakayoendelea kuongoza mapinduzi ya kidijitali hapa nchini. Tunatoa shukrani zetu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutusaidia kufanikisha mchakato huu, tunatarajia kuendelea kushirikiana kwa pamoja.


Hassanein Hirdjee, Mwenyekiti wa AXIAN Telecom.
Muungano wa AXIAN Telecom umeweka vipaumbele vinne (4) muhimu katika kutekeleza majukumu yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:

• Kuendeleza mabadiliko ya kidijitali nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa na kutoa huduma zinazowanufaisha mtumiaji mmoja mmoja na makampuni ya Kitanzania. Muungano huu una uwezo wa kutumia teknolojia za mtandao wa kasi na nyaya za chini ya ardhi ambazo zitaleta mawasiliano ya haraka kati ya Watanzania na kwingineko duniani.

• Kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za mawasiliano na kuongoza ujumuishwaji wa kidijitali kwa kuwekeza kikamilifu kwenye ujenzi wa miondombinu ya mawasiliano. Muungano huu unapanga kuimarisha upatikanaji na ubora wa mtandao hasa kupitia teknolojia ya 4G.

• Kuongeza kasi ya ujumuishwaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi, kwa kuzingatia mafanikio ya huduma hizi kutoka kwenye kampuni zilizounganishwa ili kuendeleza zaidi huduma za kifedha kwa njia ya simu zinazolenga mahitaji ya wateja wa Tanzania. Umoja huo pia utahakikisha muungano huu unafaidika kupitia utaalamu wake wa kutoa huduma za kifedha za kiwango cha juu katika nchi zingine.

• Kukuza na kuendeleza vipaji. Muungano huo unakusudia kukuza maendeleo ya taaluma za wafanyakazi na kuweka mkazo mkubwa kwenye mafunzo, kubadilishana uzoefu na kushirikishana maarifa ya pamoja miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania PLC.

Muungano huu unajumuisha AXIAN Telecom na Bw. Rostam Azizi, mtanzania mfanyabiashara na mjasiriamali ambaye ana taaluma ya muda mrefu kwenye sekta ya mawasiliano na amekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya sekta hii hapa nchini Tanzania. Bw. Azizi, akiwa kama Mwenyekiti ajaye wa MIC Tanzania PLC, atatoa mwongozo wa kimkakati na usimamizi wa kampuni na mfumo mzima wa uendeshaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wadau wa sekta ya mawasiliano nchini Tanzania.

Tulipoanza safari yetu ya mawasiliano zaidi ya miaka ishirini iliyopita, suala kubwa lilikuwa kuunganisha watanzania kwenye huduma hii. Tulikuwa waanzilishi katika kujenga mtandao wa huduma za simu, hasa katika maeneo ya vijijini, ambapo kwa sasa Watanzania wenzangu wengi wanafurahia huduma hii. Tukitazama malengo ya pamoja na AXIAN Telecom, ni Dhahiri kuwa tutafanikiwa kuondoa vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa huduma za kidigitali nchini kote, tukizingatia mahitaji muhimu kwa Watanzania na makampuni.

 

Rostam Azizi, Mwenyekitii MIC Tanzania PLC.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Katika Toleo la dhamana la AXIAN Telecom lilifanikiwa na kukamilika Februari 2022, linaashiria matumizi ya mara ya kwanza ya mfumo wa escrow kwa kampuni binafsi inayofanya kazi barani Afrika na kuakisi sifa ya Tanzania kama chaguo la wawekezaji. Mafanikio ya dhamana yanatoa ishara tosha kwa masoko yote kuwa wawekezaji wa kimataifa wana fursa za uwekezaji hapa nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla . AXIAN Telecom inafungua njia mpya kwa sekta binafsi barani Afrika kuhamasisha uwekezaji ili kuboresha maisha ya kila siku ya watu inayowahudumia.

Ikitumia utaalamu wake hasa katika kusambaza teknolojia za hali ya juu kama vile mitandao ya 5G na kuanzisha huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi zilizofanikiwa, AXIAN Telecom ina dhamira ya kuupa nguvu mfumo wa mawasiliano hapa Tanzania hasa katika kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma bora zaidi.

KUHUSU AXIAN TELECOM
AXIAN Telecom ni mtoaji wa huduma za mawasiliano barani Afrika wanaofanya kazi katika masoko manane kupitia kampuni tanzu nchini Madagascar, Comoro, Reunion, Mayotte, Senegal, Togo, Uganda na Tanzania.
Inafanya kazi katika sehemu tatu kuu za biashara, kutoa huduma za mtandao wa simu na zile zisizotumia mtandao na vile vile miundombinu ya kidijitali na huduma za kifedha kupitia simu. AXIAN Telecom inahudumia karibu wateja milioni 33 na ni kitovu kikubwa cha soko, baada ya kukua kutoka namna ilivyokuwa inafanya kazi hapo awali, kutoka kuhudumia soko moja (Madagascar) hadi 2015 kuwa na masoko manane leo, kupitia ununuzi unaoendelea na uwekezaji mkubwa wa mtandao.
Kwa utaratibu mzuri, tunahakikisha kwamba shughuli zetu za kibiashara zina matokeo endelevu na chanya na ya kudumu katika maisha ya kila siku ya mamilioni ya watu.
Pata maelezo zaidi kuhusu AXIAN Telecom: www.axian-telecom.com

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI
HABARI

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA
HABARI

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI
HABARI

WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
BIKIRA JANE APATA MTOTO
HABARI

BIKIRA JANE APATA MTOTO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA
HABARI

ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA

by ALFRED MTEWELE
Mar 21, 2023
SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO
HABARI

SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In