“Sote tumeumizwa sana na tunaumizwa kila siku na mwenendo wa matokeo ya timu yetu (Azam FC) niwaombe mashabiki wenzangu tuendelee kuwa wavumilivu shida sio mwalimu au wachezaji tatizo ni uongozi unaleta wachezaji wa daraja gani katika timu yetu, tuna wachezaji wa daraja moja tofauti yao ni nani ameamka vizuri siku ya mchezo husika”
“Hapa (Azam FC) hata aje mwalimu yoyote kwa aina ya wachezaji tulionao kuchukua ubingwa, kwa kutoa ushindani kwa timu zingine kwa sasa sio rahisi kwa mtazamo wangu, nianze na mwalimu tulie nae ni mwalimu mzuri sana kwa falsafa yake ya kupenda kucheza kwa kasi na kurudi kuja kukaba, tatizo linakuja aina ya wachezaji tulionao kuna muda wana wajibika ipasavyo na kuna muda hawawajibiki”
“Kitu muhimu ni mwalimu kupewa nafasi ya kusajili wachezaji wa aina anayoitaka angalau iwe kwa gharama kubwa wachache na wenye kuleta chachu ndani ya uwanja na kupewa muda awekeze falsafa yake kwenye timu, kitu kingine asilimia kubwa kwa sasa wachezaji wetu utimamu wa mwili ni mdogo mno wachezaji wetu wanaweza kucheza kwa kushambulia na kukaba kwa wakati dakika 45 pekee hapo mwalimu wa viungo naona hawatendei haki wachezaji wetu”
“Wachezaji wetu (Azam FC) wamekuwa sio watu wa kujitoa ndio maana leo tunamponda Kigonya kesho tunamponda Salula wachezaji hawakai kwenye kiwango kilekile kwa muda mrefu, binafsi niwaombe (Mashabiki) tupaze sauti kwa wahusika juu ya kufanywa kwa usajili wenye tija kwa timu yetu” Emmanuel Madata Lubigisa, Shabiki wa Azam FC.