Msanii wa muziki nchini Kenya, Kevin Bahati ameangua kilio mbele ya waandishi wa habari mara baada ya chama cha Jubilee kutengua uteuzi wake katika kuwania ubunge eneo la Mathare.
–
Akidondokwa na machozi, Bahati alimsihi kiongozi wa chama cha Jubilee, Rais Uhuru Kenyatta awapatie vijana fursa ya kuongoza.
–
“Hiki cheti sio tu cha Bahati, ni cha vijana wote wa Mathare. Watu wa Mathare wanahitaji kiongozi ambaye anaelewa shida zao na ambaye ameishi nao.” alisema mwimbaji huyo kuhusu cheti alichokabidhiwa siku tatu zilizopita.
–
Bahati alizaliwa na kulelewa eneo la Mathare, alitangaza nia ya kuwania wadhifa wa ubunge eneo hilo yapata mwezi mmoja uliopita.
–
Aidha, Bahati anakuwa msanii wa pili nchini humo kutupwa nje kwenye mbioni za ubunge ndani ya vyama baada ya Jaguar.