Bao la Mayele Sh50 milioni – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 16, 2022
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Bao la Mayele Sh50 milioni

I am Krantz by I am Krantz
Apr 10, 2022
in MICHEZO
0
UWEZO WA MAYELE WAMVUTA WINGA AS VITA
0
SHARES
32
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NYOTA wa Yanga wamerudi kambini jana jioni, lakini walipofika tu wamekutana na Sh50 milioni iliyopatikana kupitia bao la kiufundi la straika Fiston Mayele.

Kama uliuangalia vizuri mchezo wa Yanga na Azam juzi, takribani dakika 77 kulikuwa na vita kati ya mabeki wa kati wa Azam wakiongozwa na Aggrey Morris dhidi ya Mayele iliyokuja kuhitimishwa kwa bao hilo la pili lililoipa ushindi Yanga.

RelatedPosts

No Content Available
Load More

Iko hivi. Kama si bao hilo Yanga ilikuwa inapoteza kiasi cha Sh 50 milioni walizoahidiwa na matajiri wao GSM kama posho lakini Yanga iliposhinda tu mambo yakawa uhakika.

Katika mchezo huo Mayele na Aggrey walianza kuonyeshana kazi mapema tu wakionekana kupambana vikali kila mmoja akitafuta ubora wake.

Dakika 2, Mayele alipokea krosi ya Saido katika kuunganisha mpira huo ulionekana kuguswa na mkono wa Morris ila mwamuzi wa kati, Nassor Mwinchui hakutafsiri kama penalti na kumwacha straika huyo akilalamika.

Aggrey aliendelea kupambana kumzuia mshambuliaji huyo ambapo dakika ya 6, alimbana alipoingia ndani ya eneo la hatari na kipa wake Ahmed Salula kuuwahi na kuudaka.

Dakika ya 50 na 52 Morris aliendelea kumdhibiti Mayele akitangulia kumzuia kuingia ndani ya eneo la hatari kisha kugeuka na kutoa pasi kwa wenzake.

Kibao kilianza kugeuka dakika ya 66 Mayele aliachia shuti kali Salula akapangua na kudaka tena mshambuliaji huyo akimzidi akili Morris sambamba na Kheri.

Baada ya shambulizi hilo Mayele alimsababishia maumivu Kheri na kulazimika kutibiwa kisha baadaye kushindwa kuendelea na mchezo na kubaki na Morris uwanjani. Dakika ya 78 Aggrey alimsahau kidogo Mayele na kuchoma nyumba.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alisema hatua ya Mayele kubanwa na mabeki hao ilitokana na dosari ya viungo wake wa pembeni Dickson Ambundo na Denis Nkane kushindwa kumsaidia.

“Niliona hiyo hali ya ushindani kwangu mimi ni kitu kizuri kwa kuwa kinamjenga mchezaji lakini ile hali ingepungua kama Ambundo na Nkane wangekuwa wanafanya kazi zao kwa ukaribu kushirikiana na Mayele,” alisema Nabi.

Related

Tags: MAYELE
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

NENDENI MKAPAMBANE TAIFA LINAWATEGEMEA WACHEZAJI
HABARI

NENDENI MKAPAMBANE TAIFA LINAWATEGEMEA WACHEZAJI

by ALLY ZINGIZI
May 14, 2022
Manula Afunguka ni Wapi Atacheza Msimu Ujao..Azam Yatajwa
HABARI

Manula Afunguka ni Wapi Atacheza Msimu Ujao..Azam Yatajwa

by I am Krantz
Apr 29, 2022
Wema Sepetu Atoa Neno “Lulu Michael ni Mdogo Wangu Naweza Mpiga Hata KOFI, Mkiona Tunagombana Tulia”
BURUDANI

Wema Sepetu Atoa Neno “Lulu Michael ni Mdogo Wangu Naweza Mpiga Hata KOFI, Mkiona Tunagombana Tulia”

by I am Krantz
Apr 27, 2022
AKAUNTI YA DIAMOND YAFUTWAA YOUTUBE
BURUDANI

AKAUNTI YA DIAMOND YAFUTWAA YOUTUBE

by ALLY ZINGIZI
Apr 25, 2022
Absa Tanzania yakabidhi zawadi kwa mshindi wa kampeni ya Absa Card Assist ya ligi kuu ya Uingereza (EPL)
BIASHARA

Absa Tanzania yakabidhi zawadi kwa mshindi wa kampeni ya Absa Card Assist ya ligi kuu ya Uingereza (EPL)

by ALLY ZINGIZI
Apr 25, 2022
Mo Salah Avunja Rekodi ya Ozil Dhidi ya United
MICHEZO

Mo Salah Avunja Rekodi ya Ozil Dhidi ya United

by I am Krantz
Apr 22, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In