Beki wa Orlando Pirates Paseka Mako, anaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka hospitali alipokuwa akipatiwa matibabu tangu alipoumia Aprili 12, 2022 kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Baroka FC.
Katika mchezo huo Paseka Mako alikuwa akiokoa mpira katika eneo la hatari ndipo kipa wake Richard Ofori, alitoka nje ya eneo lake na kwenda kuvaana naye na kumpiga na goti maeneo usoni.
Mako alipoteza fahamu baada ya kuanguka wahudumu wa afya pamoja na gari la wagonja (Ambulance) viliingia uwanjani kwa ajili ya kumuwahisha hospitali.
Mchezaji huyo amefanyiwa upasuajia kichwani kwenye eneo la jicho. Hata hivyo mchezaji huyo atalazimika kujiuguza akiwa nyumbani hadi mwisho wa msimu huu.