ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, February 7, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki ya CRDB; Tuko tayari kufanya kazi na makampuni ya bima ya TAKAFUL

I am Krantz by I am Krantz
Apr 15, 2022
in BIASHARA
0
Benki ya CRDB; Tuko tayari kufanya kazi na makampuni ya bima ya TAKAFUL
0
SHARES
174
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

 

Kamishina wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Miongozo ya Bima 2022 yenye kufuata misingi ya dini ya kiislam (TAKAFUL).

 

WATEJA wa Benki ya CRDB sasa wanaweza kupata huduma za Bima zinazofata misingi ya Shariah, ijulikanayo kama Takaful baada ya kuzinduliwa kwa miongozo mipya ya Bima 2022.

 

Kuazishwa kwa huduma za bima za Takaful kunaongeza muhimili wa pili katika mfumo wa fedha unaofata misingi ya kiislam katika soko, hii imekuja baada ya takriban miaka 14 tokea huduma za kibenki zinazofata misingi ya kiislam kuanzishwa nchini, hii inaashiria muendelezo  wa ukuaji wa mfumo wa fedha wa kiislam Tanzania.

 

Kwa upande wa huduma za kibenki zinazofata misingi ya Shariah, kwa mara ya kwanza huduma hizi zinapatika nchi nzima kupitia CRDB Al Barakah Banking, ambazo zilianzishwa mwishoni mwa mwaka jana.

 

Benki hiyo imezitaka Kampuni za Takaful kuwekeza fedha katika misingi inayofata Shariah, hivyo basi benki hiyo imeyahakikishia makampuni ya Takaful kwamba, CRDB Al – Barakah ipo tayari na imejidhatiti kuwapatia fursa za uwekezaji unaofuata misingi ya Shariah.

 

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Barakah Banking, Rashid Rashid, alisema.

 

“Sisi kama Benki ya CRDB, na hususan kupitia huduma zetu za Al Barakah pamoja na kitengo cha BIMA cha CRDB, tuko tayari kufanya kazi na taasisi zitakazojisajili kutoa huduma za TAKAFUL kwa namna mbalimbali.”

 

Kwa sasa “tumefarijika sana kwamba sasa mwanga umefunguka wa kuwawezesha wateja wetu kupata huduma za BIMA zinazofata misingi ya Shariah, yaani Takaful.” Alisema Rashid.

Katika mfumo wa fedha unaofata misingi ya Halal au Shariah, kuna mihimili mikuu mitatu ambayo ni Islamic Banking, Islamic Insurance pamoja na Islamic money markets & capital markets (Masoko ya fedha na mitaji).

 

Ili mfumo wa kifedha unaofata Shariah ukamilike bado kulikuwa kunatakiwa uwepo wa Islamic Insurance (Takaful) pamoja na masoko ya fedha na mitaji, ambapo mihimili hii miwili ya mwisho haikuwepo na hivyo kupelekea benki zinazotoa huduma zinazofata Shariah kufanya miamala yake ya BIMA kwa dharura ya kutumia BIMA za conventional.

 

Ujio wa Takaful sio tu unaongeza wigo wa huduma za bima nchini, bali utazisaidia benki zinazofuata misingi ya Shariah kukidhi vigezo vya kishariah katika utoaji wa huduma zake.

 

“Wateja wote wa CRDB Al Barakah watatumia huduma za TAKAFUL katika mahitaji ya BIMA, kwa sababu hapo awali tulikua tunatumia bima za conventional kwa mlango wa dharura. Kwa ujio wa Takaful, mlango wa dharura  umefungwa, kwa hiyo tutatumia Takaful.” alisema Rashid.

 

Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Barakah Banking, Rashid Rashid, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miongozo ya BIMA 2022 yenye kufuata misingi ya dini ya kiislam (TAKAFUL) uliofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki ya CRDB.   (Na Mpigapicha Wetu).

 

Mkuu wa Kitengo cha CRDB kinachosimamia  masuala ya BIMA, Moureen Majaliwa, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Miongozo Mipya ya BIMA ya TAKAFUL. 


Kamishina wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Miongozo ya BIMA 2022 yenye kufuata misingi ya dini ya kiislam (TAKAFUL). 

 

RelatedPosts

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

Aug 9, 2022

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA

Aug 2, 2022

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAKANDARASI NA WAZABUNI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEZESHAJI KUTOKA BENKI YA CRDB

Jul 21, 2022
Load More
 
Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Barakah Banking, Rashid Rashid (kushoto) akibadilisha mawazo na Kamishina wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Baghayo Saqware mara baada ya uzinduzi wa Miongozo ya BIMA 2022 yenye kufuata misingi ya dini ya kiislam (TAKAFUL). 
  
Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Barakah Banking, Rashid Rashid, akizungumza na wadau wa BIMA  wakati wa uzinduzi wa Miongozo ya BIMA 2022 yenye kufuata misingi ya dini ya kiislam (TAKAFUL).

Related

Tags: CRDB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

NMB yafadhili ziara ya mafunzo Machinga, Bodaboda Dar nchini Rwanda
BIASHARA

NMB yafadhili ziara ya mafunzo Machinga, Bodaboda Dar nchini Rwanda

by I am Krantz
Feb 3, 2023
Benki ya NMB Yakabidhi Tiketi kwa Viongozi 12 Kwenda Rwanda na Kurudi
BIASHARA

Benki ya NMB Yakabidhi Tiketi kwa Viongozi 12 Kwenda Rwanda na Kurudi

by ALFRED MTEWELE
Feb 3, 2023
TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA CEMENT UJENZI WA KITUO CHA POLISI KIBURUGWA
BIASHARA

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA CEMENT UJENZI WA KITUO CHA POLISI KIBURUGWA

by Ally Hamis Zingizi
Jan 27, 2023
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAIPIGA JEKI SEKTA YA ELIMU YATOA MSAADA WA MIFUKO 150 YA CEMENT KUBORESHA MADARASA
BIASHARA

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAIPIGA JEKI SEKTA YA ELIMU YATOA MSAADA WA MIFUKO 150 YA CEMENT KUBORESHA MADARASA

by Ally Hamis Zingizi
Jan 27, 2023
TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KATA YA GOWEKO
BIASHARA

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KATA YA GOWEKO

by Ally Hamis Zingizi
Jan 27, 2023
Benki ya NBC Yahitimisha Kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’
BIASHARA

Benki ya NBC Yahitimisha Kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’

by ALFRED MTEWELE
Jan 27, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In