Benki ya NMB yakusanya Bil. 74.3 kupitia Hati Fungani ya ‘NMB Jasiri’  – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, May 19, 2022
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki ya NMB yakusanya Bil. 74.3 kupitia Hati Fungani ya ‘NMB Jasiri’ 

I am Krantz by I am Krantz
Apr 28, 2022
in HABARI
0
Benki ya NMB yakusanya Bil. 74.3 kupitia Hati Fungani ya ‘NMB Jasiri’ 
0
SHARES
33
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

May 19, 2022

NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

May 19, 2022

NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

May 19, 2022
Load More

 

Naibu Katibu Mkuu – Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru, akigonga kengele kama ishara ya kuorodheshwa rasmi ‘NMB Jasiri’ kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni; Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) – Moremi Marwa(Kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB- Ruth Zaipuna na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama (Kulia).

Naibu Katibu Mkuu – Sera,  Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji – CPA Nicodemus D. Mkama, Mkurugenzi Mkuu wa DSE- Moremi Marwa,  Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna, Afisa Mkuu waFedha Benki ya NMB – Juma Kimori pamoja na wawakilishi kutoka FSD Africa, Ubalozi wa Uingereza, International Finance Co-operation (IFC), Orbit Securities Ltd na UN Women wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kuorodhesha hati fungani ya NMB Jasiri  katika Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE). 

 

Benki ya NMB imefunga mauzo ya Hati Fungani ya Jasiri (NMB Jasiri Bond) kwa mafanikio makubwa Iliyoweka rekodi ya makusanyo Afrika Mashariki na Kati ya Sh. Bil. 74.27 na kuvuka lengo la Sh. Bil. 25, ufungaji ulioenda sambamba na kuiorodhesha rasmi hati hiyo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Hafla hii ilihudhuriwa na Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu- Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru aliyemwakilisha Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande, ametangaza rasmi kuorodhozeshwa kwa hati fungani ya Jasiri na sasa kuanza kununuliwa na kuuzwa kupitia soko la hisa la Dar es salaam.

Akizungumza Mafuru aliipongeza NMB kwa ubunifu chanya wa Jasiri Bond, hati fungani iliyolenga kukusanya fedha ili kutoa mikopo kwa biashara ndogo ndogo na za kati zinazo milikiwa au kuongozwa na wanawake na biashara ambazo bidhaa au huduma zake zinamgusa mwanamke moja kwa moja. 

 “Hii sio mara ya kwanza kwa NMB kuja na Hati Fungani na kuvuka lengo la makusanyo, hii ni mara ya nne na kwa hati hii ambayo ni ya kipekee, kama jina lake lilivyo, kumekuwa na ujasiri mkubwa sana, kwani jina Jasiri linaashiria mambo mengi sana.

“Ujasiri wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), ya kuiruhusu Hati Fungani hii kuingia sokoni kabla hata ya sheria zake hazijawa tayari, jambo linalothibitisha imani ya mamlaka hii kwa NMB ilivyokuwa kubwa.

 “Lakini pia, NMB ikalenga kupata Sh. Bil. 25 na hatimaye inafunga mauzo ikiwa imepata zaidi ya mara tatu ya lengo, hii ni kuthibitisha kwamba kuna nguvu kubwa ya kiuchumi miongoni mwa wanawake, tunachotakiwa ni kuweka mazingira wezeshi ya kuwaamini kama wenzetu NMB walivyofanya,” alisisitiza Mafuru.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema NMB ilipokea maombi 1,630 yaliyowezesha kukusanya Sh. Bil. 74.27 badala ya Bil. 25 na kuwashukuru wateja na wawekezaji wote kwa kuiamini benki hio. 

“Kuaminika kwa NMB katika hili kunathibitishwa na kuwa asilimia 96 ya waliotuma maombi ya kununua Hati Fungani, yamepitia katika matawi yetu, huku asilimia 4 tu yakifanyika kupitia Madalali wa Soko la Hisa waliosajiliwa”.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA), Nicodemus Mkama, aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa NMB, kwa kufanikisha uuzwaji wa ‘Jasiri Bond’ kwa Umma wa Watanzania na hatimaye kufikia hatua ya kuiorodhesha DSE, tayari kwa mauzo ya walionunua na manunuzi ya waliokosa katika mchakato uliofungwa.

Wengine waliohudhuria hafla hii ni Mkurugenzi Mkuu WA DSE, Moremi Marwa, pamoja na wawakilishi kutoka FSD Africa, Ubalozi wa Uingereza, International Finance Co-operation (IFC), UN Women na Orbit Securities Ltd.

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA
BIASHARA

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU
HABARI

NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

by I am Krantz
May 19, 2022
“PANYA ROAD” KAENI CHONJO SERIKALI IPO KAZINI
HABARI

“PANYA ROAD” KAENI CHONJO SERIKALI IPO KAZINI

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
RAIS SAMIA AMETOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU-MAJALIWA
HABARI

RAIS SAMIA AMETOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU-MAJALIWA

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO
BIASHARA

WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
TUMEUMIZWA NA MATOKEO YA JANA – AHMED ALLY
HABARI

TUMEUMIZWA NA MATOKEO YA JANA – AHMED ALLY

by Shabani Rapwi
May 19, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In