Breaking : SERIKALI YATANGAZA AJIRA ZA AFYA 7,612, UALIMU 9,800… SOMA VIGEZO HAPA…. – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 16, 2022
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Breaking : SERIKALI YATANGAZA AJIRA ZA AFYA 7,612, UALIMU 9,800… SOMA VIGEZO HAPA….

MWISHO KUTUMA MAOMBI MEI 4

I am Krantz by I am Krantz
Apr 21, 2022
in HABARI
0
Breaking : SERIKALI YATANGAZA AJIRA ZA AFYA 7,612, UALIMU 9,800… SOMA VIGEZO HAPA….
0
SHARES
37
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) imepata kibali cha ajira za Watumishi wa Kada za Afya 7,612 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Ualimu 9,800 wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hivyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 20 Aprili – 04 Mei, 2022.

RelatedPosts

No Content Available
Load More

Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree).

A: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA ZA UALIMU

Walimu wote wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz.

Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Kozi za Ualimu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2021. Waombaji ambao waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo wa maombi ya ajira wanatakiwa kuomba upya.

1.0 SIFA ZA WAOMBAJI

1.1 SIFA ZA KITAALUMA ZA MWOMBAJI

Walimu wanaotakiwa kutuma maombi wawe na sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:

1.2 WALIMU WA SHULE ZA MSINGI

Walimu wanaoomba kuajiriwa kufundisha Shule za Msingi wawe na sifa zifuatazo:

i. Mwalimu Daraja la III A – Mwenye Astashahada ya Ualimu Elimu ya

Msingi (Certificate in Primary Education);

ii. Mwalimu Daraja la III B – Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu ya Awali;

iii. Mwalimu Daraja la III B – Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu ya Msingi;

iv. Mwalimu Daraja la III C – Mwenye Shahada ya Ualimu kwa Elimu ya

Awali; na

v. Mwalimu Daraja la III A, III B na III C – Mwenye Astashahada,Stashahada na Shahada ya Ualimu (Elimu Maalum) kwa masomo ya Lugha na Sanaa.

1.3 WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI

i. Mwalimu Daraja la III B – Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu Maalum kwa masomo ya English Language, Geography, History, Kiswahili, Biology, Chemistry, Physics na Mathematics;

ii. Mwalimu Daraja la III C – Mwenye Shahada ya Ualimu aliyesomea Elimu Maalum kwa masomo ya English Language, Geography, History, Kiswahili, Biology, Chemistry, Physics na Mathematics;

iii. Mwalimu Daraja la III B – Mwenye Stashahada ya Ualimu wa somo la Biology, Chemistry, Physics na Basic Mathematics;

iv. Mwalimu Daraja la III C – Mwenye Shahada ya Ualimu somo la Physics,Mathematics, Chemistry na Biology;

v. Mwalimu Daraja la III C – Mwenye Shahada ya Ualimu wa somo la English Language, English Literature, Chinese Language, French Language na Kiswahili;

vi. Mwalimu Daraja la III C – Mwenye Shahada ya Ualimu somo la Commerce, Accountancy na Economics;

vii. Mwalimu Daraja la III B – Mwenye Stashahada ya Ualimu Elimu somo la

Book Keeping na Commerce;

viii. Mwalimu Daraja la III C – Mwenye Shahada ya Ualimu kwa masomo ya

General Studies, History na Geography;

ix. Mwalimu Daraja la III B – Mwenye Stashahada ya Ualimu kwa masomo

ya Civics, History, Geography, English Language na Kiswahili;

x. Mwalimu Daraja la III C – Mwenye Shahada ya Elimu ya Michezo

(Bachelor of Science in/ with Physical Education); na

xi. Mwalimu Daraja la III B – Mwenye Stashahada ya Elimu ya Michezo

(Diploma in Physical Education).

B: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA KADA ZA AFYA

Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia

kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. Waombaji ambao waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo wa maombi ya ajira wanatakiwa kuomba upya.

2.0 Sifa za Waombaji ni kama ifuatavyo:-

2.1 DAKTARI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Waombaji wawe wamemalizamafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

2.2 DAKTARI WA MENO DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

2.3 TABIBU DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2.4 TABIBU WA MENO DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya Tabibu Meno (Diploma in Clinical Dentistry) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2.5 TABIBU MSAIDIZI

Waombaji wawe wamehitimu Astashahada ya miaka miwili ya Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistant Certificate) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2.6 MFAMASIA DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Famasi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali waliohitimu mafunzo kwa vitendo (Internship) ya mwaka mmoja na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).

2.7 MTEKNOLOJIA (DAWA) DARAJA II

Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Dawa (Diploma in Pharmaceutical Technology) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).

2.8 MTEKNOLOJIA (MAABARA) DARAJA II

Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Diploma in Health Laboratory Science) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).

2.9 MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (MAABARA) 

Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Certificate in Health Laboratory Science) kwa muda wa miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).

2.10 MTEKNOLOJIA (MIONZI) DARAJA II

Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Mionzi (Diploma in Radiology/Radiography) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo

kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wawe wamesajiliwa na Baraza la

Wataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology and Imaging

Professionals Council)

2.11 AFISA MUUGUZI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo kwa vitendo (Internship) ya mwaka mmoja ambao wamesajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurses and Midwifery Council).

2.12 AFISA MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).

2.13 MUUGUZI DARAJA LA II

Waombaji wawe na cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la

Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council)

2.14 FUNDI SANIFU VIFAA TIBA II

Waombaji wawe na Stashahada ya kawaida ya Ufundi (Full Technician Certificate) ya miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2.15 AFISA AFYA MAZINGIRA MSAIDIZI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira ya miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Afya ya Mazingira (The Environmental Health Practitioners’ Registration Council).

2.16 MSAIDIZI WA AFYA

Waombaji wawe wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu Mafunzo ya Mwaka mmoja katika fani ya Afya, Afya Ngazi ya Jamii au mafunzo yoyote yanayofanana na hayo kutoka vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali.

2.17 KATIBU WA AFYA DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Uongozi wa Huduma za Afya (Health Services Administration) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.

2.18 AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Social Work, Sociology, Psychology, Social Protection, Guidance and Counceling, Theology, Divinity, Child Protection, Social Policy, Early Childhood Development, Social Gerontology, Dietetics au fani nyingine zinazofanana na Ustawi wa Jamii kutoka Chuo cha Elimu ya Juu kinachotambuliwa na Serikali.

.19 AFISA LISHE DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi ya Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc – Nutrition, Home Economics and Nutrition, Food Science and Technology, Food Science) au Stashahada ya Juu ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition) kutoka Chuo cha Elimu ya Juu kinachotambuliwa na Serikali.

3.0 MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI

i. Awe raia wa Tanzania;

ii. Awe na umri usiozidi miaka 45;

iii. Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato cha

Nne, Sita, Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au Leseni hai ya

kufanya kazi ya taaluma husika);

Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya

Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;

v. Waombaji walioajiriwa kwa mkataba wa ajira kutoka kwa Wadau wa

Maendeleo katika Sekta ya Afya wanatakiwa kuambatisha nakala za

mkataba na barua za uthibitisho kutoka kwa Wakurugenzi wa

Halmashauri husika;

vi. Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi

wa Umma;

vii. Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIN); na

viii. Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.

4.0 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE

i. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi katika Halmashauri/Vituo

watakavyopangiwa;

ii. Waombaji wawe tayari kufanya kazi na Mashirika au Taasisi zilizoingia

Ubia na Serikali;

iii. Baada ya kupangiwa kituo cha kazi, hakutakuwa na nafasi ya

kubadilishiwa kituo cha kazi;

iv. Waombaji wote wahakikishe wanajaza taarifa zao na kuambatisha

nyaraka zote muhimu katika mfumo; na

v. Maombi ya ajira ni bure.

5.0 WAHITIMU WALIOSOMA NJE YA NCHI

i. Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi EQ… kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ili kuwawezesha kuingia kwenye Mfumo wa Ajira; na

ii. Waombaji waliosoma Vyuo vya Nje ya Nchi wanatakiwa kupata Ithibati ya

masomo yao kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili vyeti vyao

viweze kutambuliwa na kupata uhalali wa kutumika hapa nchini.

Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa

maombi kwa nafasi za Kada za Afya na Elimu, tafadhali bofya: www.tamisemi.go.tz au

wasiliana na Kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba

za simu 026 2160210 au 0735 160210.

Waombaji wenye Ulemavu na sifa zilizoainishwa katika tangazo hili watume

maombi yao ya kazi kwa nakala ngumu (hard copy). Maombi yao yaeleze aina ya

ulemavu wao na kuambatisha picha zao na yatumwe katika anwani ifuatayo:

Katibu Mkuu,

Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira & Wenye Ulemavu)

S.L.P.980,40480 DODOMA (Aione: Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu Wenye

Ulemavu)

Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa

moja Ofisini hayatafanyiwa kazi. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe

04 Mei, 2022 saa 05:59 usiku. Tangazo hili linapatikana katika tovuti ifuatayo:

www.tamisemi.go.tz

Limetolewa na: Katibu Mkuu,

Ofisi ya Rais – TAMISEMI,

Mji wa Serikali – Mtumba,

S.L.P 1923,

41185 DODOMA.

Aprili 20,2022.

Unaweza kupakua PDF <<hapa>>

Related

Tags: AjiraNAFASI ZA KAZI
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE
HABARI

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E
HABARI

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU
HABARI

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
JOSE PESEIRO KOCHA MPYA WA NIGERIA
HABARI

JOSE PESEIRO KOCHA MPYA WA NIGERIA

by SHABANI RAPWI
May 16, 2022
SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI
HABARI

SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI

by I am Krantz
May 16, 2022
UKRAINE YATAKA KUUNGWA MKONO NA AFRIKA KATIKA VITA NA URUSI
HABARI

UKRAINE YATAKA KUUNGWA MKONO NA AFRIKA KATIKA VITA NA URUSI

by SHABANI RAPWI
May 16, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In