Mwanamuziki mashuhuri nchini Tanzania, Diamond Platnumz, anatarajia kuachia album yake ya nne katika maisha yake ya muziki baada ya kupata mafanikio makubwa na album ya ‘A Boy From Tandale’ aliyoiachia mwaka 2017.
–
Akizungumzia ujio wa album hiyo, Diamond Platnumz amemtaja producer mkubwa wa muziki kutoka Marekani Swizz Beatz kuwa ndio mtayarishaji mkuu wa album yake ijayo, ameeleza hayo akiwa nchini Uingereza kupitia Podcast ya Afrobeats inayoongozwa na Adesope.
–
Huu unakuwa ni muendelezo wa Swizz Beatz kufanya kazi pamoja na Diamond pia akiwa ni msanii wa kwanza toka Afrika kutayarishiwa album na Swizz Beatz.
–
Mathalani mwaka 2020 Diamond alishirikishwa kwenye album ya Alicia Keys ‘ALICIA’ na kusikika kwenye wimbo uitwao Wasted Energy. Album hiyo ya Alicia ilitayarishwa na mumewe Swizz Beatz.
–
Ilifanikiwa kushika namba moja kwenye chati za Billboard upande wa ‘Top R&B Albums’ mara ya baada ya kufanya vizuri katika mauzo.