Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi kinachorushwa kwenye kituo cha radio Wasafi FM, Diva Thee Bawse ameweka wazi kupata ajali ya gari pamoja na mumewe Abdulrazak Salum.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram amethibitisha hilo kwa ku-share video fupi (clip) na kutoa taarifa kwamba wote wapo salama.
“Asante kwa raia waliotusaidia with alot of love maana i was devastated .. and thanks @iamnellyg5 Ni Mungu tu!. leo tunaendelea na matibabu …. maisha ya Mwanadamu ni mafupi sana nimeona jana. bajaj au Pikipiki wakiendelea achiwa wataendelea sababisha vifo vya wengi sana.
“Siwez ata kulala naona ile bajaj ikipanda juu ya kioo cha gari and the blood … it was scary Mungu wangu🥲 ila Mungu anatupenda sana Kwa Ule mzinga tumetoka wazima Ni kudra zake mwenyezi Mungu na msaada tumepata kwa mapenzi sana makubwa ya watu.
“Nimepost kushukuru watu raia wa kawaida kabisa ambae walitu take care na kuhakikisha kila kitu chetu kiko salama na sisi tuko salama hatuna cha kuwalipa kabisa zaid ya shukran za upendo kwenu!”
“Pole sana Mume Wangu Abdulrazak Salum as long as we alive means we still have a long way to go…praying for you … for a full recover” Ameandika Diva.