Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amewataka baadhi ya wabunge kuacha tabia kutumia vishkwambi vya wabunge wengine kutoa michango
Dkt. Tulia amesema hayo Leo Aprili 21,2022 Bungeni jijini Dodoma baada ya kuhitimisha kipindi cha maswali na majibu
Spika Dkt. Tulia amesema kitendo cha Mbunge kutumia kishkwambi cha mbunge mwengine inaamaanisha kwamba taarifa hiyo imetolewa na mbunge anayemiliki kishikwambi hicho
“Kuna wataalamu wetu ambao wanazunguka Bungeni wakati wote kwa hiyo kama kishkwambi chako kinashida waambie watakusaidia,unapotoa taarifa Kwa kutumia kishkwambi cha mbunge mwenzako mchango huo unaonekana wa mbunge huyo uliyetumia kishkwambi chake” amesema Dkt.Tulia Ackson