Tajiri namba moja duniani Elon Musk aingia kwenye vikwazo vya kuununua mtandao wa Twitter baada ya bodi ya wakurugenzi wa mtandao huo kujihami dhidi ya kile, kwa kile ilichokiita “ununuzi wa shari” ikiwa ni siku kadha Elon Musk kutangaza ofa ya kuununua mtandao huo.
Elon Musk ni mmoja wa wawekezaji mwenye asilimia 9.2 ya hisa kwenye mtandao huo, alitangaza ofa ya dola bilioni 43 ambazo ni takribani Shilingi Trilioni 94.5 ili kuununua Twitter kwa asilimia 100.
Hatua ya bodi ya wakurugenzi wa Twitter kujihami dhidi ya ununuzi huo inawapa nafasi wawekezaji wote wa mtandao huo kumiliki asilimia 15 ya hisa na si zaidi ya hapo.
Bodi ya wakurugenzi ya Twitter imeelezea kwa kina mpango wake wa kujilinda na ununuzi huo kwa tume ya Ulinzi wa Mali na Mbadilishano ya Marekani na kutoa taarifa kuwa ilihitaji kuchukua hatua hiyo kwasababu ya pendekezo la Musk walilodai “halikuwa ombi, halishikamani na taratibu za kuimiliki Twitter”.