Elon Musk amenunua 9.2% ya hisa za kampuni ya Twitter, kulingana na jalada la dhamana la Marekani.
Taarifa hiyo ilifanya thamani ya hisa za Twitter kupanda kwa 25% kabla ya soko la hisa kufunguliwa.
Mwanzilishi huyo wa Tesla falinunua hisha 73,486,938 za Twitter mnamo Machi 14, kulingana na Tume ya Kubadilishana Dhamana.
Dau hilo lina thamani ya $2.89bn (£2.20bn), kulingana na bei ya mwisho ya Twitter siku ya Ijumaa.
Hisa hizo zinamfanya kuwa mmoja wa wanahisa wakubwa katika kampuni hiyo na ni zaidi ya mara nne ya 2.25% ya mwanzilishi wa Twitter Jack Dorsey.
Musk ni mtumiaji wa kawaida wa Twitter aliye na wafuasi zaidi ya milioni 80, ingawa hivi majuzi alisema “anafikiria sana” kuunda jukwaa mpya la mtandoa wa kijamii.
Mwishoni mwa mwezi uliopita Musk aliuliza wafuasi wake ikiwa wanafikiri mtandao wahimiza una uhuru wa kujieleza.
“Uhuru wa kujieleza ni muhimu kwa demokrasia inayofanya kazi.
Je, unaamini Twitter inafuata kanuni hii kwa dhati?” Kisha akauliza “Je, jukwaa jipya linahitajika?”