Ikiwa ni siku chache zimepita tangu mtoto Sporal Sambalya mwenye umri wa miaka 6 kujeruhiwa na fisi mjini Bariadi mkoani Simiyu mtoto mwingine mwenye umri wa miaka 5 amenusurika kujeruhiwa na fisi majira ya saa 4 asubuhi alipokua eneo la shule ya msingi Mwabalange Mara baada ya kuachana na baba yake aliyemsindikiza shuleni hapo.
Inaelezwa kuwa mara baada ya baba huyo kumuona fisi akimvizia mwanae alipiga kelele kuwaita wananchi wengine ambao walimkimbiza fisi huyo hadi mapangoni na kuamua kumfata hadi pangoni ambako walifanikiwa kupambana nae na kumuua.

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange amesema kupatikana kwa fisi huyo ni matokeo ya operesheni za kuwasaka fisi kwenye mapango ya mjini Bariadi operesheni ambayo mbali na kufanywa mapangoni katika kata zote za mji wa Bariadi zimeendelea na operesheni hiyo hali iliyofanya fisi wakimbilie maeneo ya nje ya mji.
Ili kuhakikisha usalama wa watoto mkuu wa wilaya ya Bariadi ametoa wito kwa wazazi kuendelea kuwasindikiza watoto wao shule.
( Credit – Azam TV )