Google imetangaza nafasi za kazi zaidi ya 100 nchini Kenya baada ya kufungua kituo chake cha kwanza cha kuendeleza bidhaa (product development centre) Afrika kilichopo jijini Nairobi.
Hatua hiyo imetokana na uamuzi wa kampuni hiyo kuwekeza $ 1 bilioni (TZS trilioni 2.3) Afrika ndani ya miaka mitano ijayo katika miradi ambayo itawezesha upatikanaji wa huduma za intaneti za kasi, uhakika na nafuu.
Katika kituo hicho Google inakusudia kuajiri ‘Engineering Manager, Product Manager, Software Engineer, Senior UX Designer au UX Researcher’.
Katika taarifa yake Google imeeleza kwamba inatafuta watu wenye vipaji, ubunifu ambao watawezesha kupatikana ufumbuzi wa changamoto za kiufundi kama vile kuboresha matumizi ya simu janja kwa watu barani Afrika au kuunda bidhaa zitakazowezesha ukuaji jumuishi wa wananchi.