Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amezuru na kusali katika kaburi la mtoto Joseph Juma (4) aliyefariki Aprili 18 katika Kijiji cha Lyabukande halmashauri ya Shinyanga baada ya kupigwa na kisha kumwagiwa maji ya moto yaliyomsababishia majeraha na mwishowe kupoteza maisha.
Akiwa katika eneo hilo la kaburi Dkt. Gwajima ameagiza kukamatwa kwa majirani wa nyumba aliyokuwa akiishi marehemu Joseph Juma ambao wamekimbia kwa madai kuwa walikuwa wakishuhudia mateso yaliyokuwa yakitokea kwa muda mrefu.
Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amesema Serikali inaendelea na juhudi za kutoa elimu pamoja na kudhibiti matukio hayo.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT