ADVERTISEMENT
Ameandika mchambuzi wa soka, Oscar Oscar kuhusu makasiriko ya baadhi ya watu baada ya msemaji wa Yanga SC, Haji Manara kuvaa jezi ya Orlando Pirates.
“Kuna muda unaweza kudhani unampiga sana Haji Manara, kumbe ndio kwanza unampa bonge la promo tena BURE”
–
“According to Cambridge dictionary, the saying ‘any publicity is good publicity’ or ‘there’s no such thing as bad publicity’ is said to emphasize that it is better that something receives bad publicity than no publicity at all”
“The only thing worse than being talked about is not being talked about. Haji anaakili nyingi sana ambazo watu wengi wanaompinga HAWANA !”
–
“Anajua ku-provoke, akisubiri reaction. Anajua kujitofautisha kwenye kundi kubwa ili aongeze thamani yake sokoni. Kila mtu akicheza ‘game’ yake kwenye nafasi yake, anaweza kutoboa sokoni. Usimchukie jamaa, CHUKUA NOTES”
–
“Mimi ningekuwa sehemu ya wanaomchukia, ningemchunia kwenye kila kitu. Akiisema vibaya timu yangu, ningempuuza. Akivaa kimasai ndiyo kabisa ningemuweka kushoto !”
–
“Haji anacheza na akili zenu, na mnaomchukia ndiyo mnaoongoza kwa kusambaza hoja zake bila hata malipo. Unampa promo ya bure, halafu unakuja kutufundisha namna ya kufanya promo ili tupate pesa !”
–
“Njia nzuri ya kujitenga na mtu anaye kukera ni KUM-BLOCK. Nikumpotezea ! Njia nzuri ya kuachana na mtu anayekukera ni kumpuuza tu ! Nasikitika kuona baadhi ya watu wanaomchukia Haji, ndiyo kwanza wanaongoza kwa kumpost kila siku !… There is no such thing as bad publicity than no publicity at all”
–
“Haji ni rafiki yangu, Haji ni kaka yangu na tunaheshimiana sana. Akikosea kitu kwa nature ya kazi yangu, nitamkosoa. Akipatia kitu kwa nature ya kazi yangu, nitampongeza.”
–
“Again, njia nzuri ya kumuepuka mtu usiyempenda ni kujitenga naye. Kama bado unamfatilia, kama bado una-mpost kila siku, basi wewe bado unamkubali mmasai mpya mjini”
–
“Wito wangu kwa vijana Wenzangu, tujitahidi sana kutafuta pesa kwa bidii, zinasaidia kupunguza MAKASIRIKO. ‘The only thing worse than being talked about is not being talked about’.”
–
“Bado tuko kwenye nchi ambayo hata mwandishi wa kitabu cha ‘How to become Rich’ naye anasota kama sisi tu !”
“Mbona jana alivyovaa nguo za kimasai hamkusema kuna kosa la BRANDING ?”
ADVERTISEMENT