Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Taifa Kenani Kihongosi amewataka vijana wa chama hicho kujitokeza kuwania nafasi ya uongozi katika nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho huku akionya suala la rushwa.
Kenani ameyasema hayo baada ya kushiriki zoezi kukimbia (Jogging) na vijana wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha vijana kujitokeza katika zoezi la sensa ya watu na makazi litakalo anza hivi karibuni.
Aidha amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kwa vitendo kuwapa nafasi vijana katika uongozi na hivyo ni wakati wa vijana kujitokeza na kuunga mkono kataika kzi nzuri anzozifanya kwa maendeleo ya taifa letu.
Kenani yupo mkoani Kilimanjaro ambapo badae atazindua nyumba ya makazi ya katibu wa UVCCM wilaya ya Moshi na Rombo.