Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Elia Kadiro mwenye umri kati ya miaka 27 na 30 aliyekuwa anajishughulisha na ubebaji mizigo katika soko la Mashine Tatu mkoani Iringa amekutwa amekufa kwenye shamba alilokwenda kufanya kazi ya kibarua cha kupalilia mazao.
Kwa mujibu wa mmiliki wa shamba hilo, Rehema Mgaya, aliugundua mwili wa Kadiro ukiwa umeanza kuharibika alipokwenda kuvuna maharage kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Mwili huo umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya taratibu za maziko.
( Credit – Azam TV)