ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Wednesday, March 22, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

KINANA ATOA ONYO ZITO

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
Apr 25, 2022
in HABARI
0
KINANA ATOA ONYO ZITO
0
SHARES
172
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

 

RelatedPosts

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

MECHI ZITASIMAMA EPL KUPISHA ‘IFTAR’

Mar 21, 2023

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

Mar 21, 2023

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

Mar 21, 2023
Load More

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdurahamani Kinana amewaonya wanachama wa Chama hicho wanaotumia njia zisizokubalika ikiwemo fedha ili kuchaguliwa waache kwa sababu chama hakitawavumilia kwa kua ni kinyumr na kanuni zilizopo

Kinana ametoa onyo hilo Wilaya Mkuranga Mkoani Pwani huku kukiwa tayari michakato mbalimbali ya uchaguzi imeanza katika ngazi mbalimbali nchini kote

“Uchaguzi unaendelea hadi mei 15 mwaka huu katika ngazi mbalimbali na ngazi za chini ndiko ziliko nguvu za Chama kwenye matawi Kata na Wilaya sasa ni vema tuwe makini Ili tupate viongozi wa kweli”amesema Kinana na kuongeza

“Utakuta mtu hajawahi kuwatembelea wananchi na wala hana nia yakweli ya uongozi lakini anajitokeza wakati wa uchaguzi kuomba nafasi kwakutumia pesa au maneno ya kumharibia mtu mwingine Ili asichaguliwe hilo watu wa aina hiyo msiwakubali majina yao leteni “.

Kinana amesema kazi ya CCM ni kuwasikiliza wananchi, kuwasemea na kuwasaidia juu ya changamoto walizonazo na si kuangalia maslahi binafsi na pia amewataka viongozi kuwa makini na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kufuata misingi iliyopo na kama mtu atabainika kupata nafasi kwa njia za udanganyifu taratibu zifuatwe.

“Kama kuna mtu ataona kuwa ameonewa kuna maeneo ya kupeleka malalamiko kwakufuata utaratibu lakini ni vema uchaguzi ufanyike kwa kufuata taratibu zilizopo”alisema.

 

Kuhusu ombi la Mmoja wa viongozi wa ngazi za matawi kulipwa posho lililowasilishwa na Mmoja wa viongozi Mwajuma Nasoro, Kinana amesema huo utaratibu ulikuwepo hivyo atafuatilia Ili suala hilo lifanyiwe kazi.

ADVERTISEMENT

Akisoma taarifa ya CCM Pwani, katibu wa chama hicho mkoani humo Saidi Goa amesema Chama hicho hivi sasa pamoja na mambo mengine kina mipango wa kuboresha vitega uchumi Ili kuepukana na misaada yenye masharti.

“Tunampango wa kukamilisha Ujenzi wa uwanja maeneo ya sabasaba Kibaha na ukumbi wa Mkutano na sherehe ambazo zitakuwa zinatuingizia kipato cha uhakika”amesema Goa

ADVERTISEMENT

Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amebainisha katika mipango ya kuboresha sekta mbalimbali Mkoa huo umeweza kurejesha jumla ya wanafunzi 269 waliokuwa wamekatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito.

Kunenge ametaja mafanikio ni pamoja na kuendelea kutoa elimu bila malipo ambapo kwa kipindi cha mwaka 2021 jumla ya sh. Bil 8. 72 zilipokelewa huku mwaka 2021/2022 hadi kufikia Februari tayari sh, Bil .6.94 zilitolewa na zinatafaisha wanafunzi 483,128

“Mheshimiwa Makam Mwenyekiti hii sasa inajibu hoja na tetesi ya upotoshaji uliokuwa unasemwa kwamba Serikali sasa haisomeshi, haitoi fedha lakini sisi tunawahakikishia kwamba Serikali inaendelea kufanya jukumu hili”amesema Kunenge.

 

Kuhusu maswala ya uchumi Kunenge amebainisha mpaka sasa Mkoa una jumla ya viwanda 1453 ambavyo vimeongeza ajira na kukuza uchumi na mpaka sasa wameendelea kutenga maeneo ya uwekezaji.

Aidha Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega amemuomba Kinana kuwasilisha kwenye vikao vya ngazi za juu ombi la wakazi wa Wilaya hiyo juu ya upanuzi wa barabara ya kutoka Daresalaam kuelekea mikoa ya kusini kuwa ya njia nne Ili kupunguza adha ya foleni ambayo wamekuwa wakiipata.

Related

ADVERTISEMENT
Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Related Posts

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI
HABARI

AFUNGIWA MIAKA 40 KUTOINGIA UWANJANI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA
HABARI

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KENYA

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI
HABARI

WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI WATOA MWILI WA MAREHEMU NA KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
BIKIRA JANE APATA MTOTO
HABARI

BIKIRA JANE APATA MTOTO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023
ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA
HABARI

ASKARI ANAYETUHUMIWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE ASOMEWA MASHTAKA

by ALFRED MTEWELE
Mar 21, 2023
SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO
HABARI

SEVILLA YAMFUTA KAZI KOCHA JORGE SAMPOLI NA KUMTEUA KOCHA HUYO

by Shabani Rapwi
Mar 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In