Kocha wa timu ya Orlando Pirates, Fadlu Davids amesema Simba ni timu ngumu na hatari hasa wanapocheza nyumbani na wanatakiwa kujiandaa sawasawa kabla ya mchezo huo.
“Tunakwenda kukutana na timu nzuri, timu inapofuzu hatua hii ni lazima uipe heshima ya ubora Simba wako vizuri sana wanapocheza nyumbani,”
ADVERTISEMENT
“Simba wana washambuliaji wenye kasi. Hatutakiwi kufanya makosa mengi hatarishi, tumeshaanza kujipanga kabla ya kuanza safari.” amesema Davids.
Orlando pirate watavaana na Simba siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Beanjamini Mkapa, Dar es Salaam.
ADVERTISEMENT