Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kunachangamoto kadhaa katika chaguzi za chama hicho za mashina na hivyo kudumaza demokrasia ndani ya chama.
–
Rais Samia amesema hayo leo 30 Aprili aliposhiriki katika uchaguzi wa viongozi wa Shina namba 1 la CCM Chamwino Ikulu Jijini Dodoma.
–
“Tunakwenda na uzoefu wa wazee maarufu kupanga watu katika maeneo, hawa Watu ni wachapa kasi au siyo wachapakazi, lakini ni Mzee maarufu ana sauti kwenye eneo basi anachukua watu kupanga watu na kufifiisha demokrasia ndani ya Chama kuacha watu watoe hiyari yao katika uchaguzi Chama”
–
Aidha amesema kuna baadhi ya Viongozi kwenye matawi wamekuwa wakiwanyima fomu wagombea jambo ambalo amesema limekuwa likijitokeza kwenye chaguzi nyingi na amemtaka Katibu Mkuu Daniel Chongolo na sekretarieti yake kulishughulikia suala hilo katika chaguzi zijazo.
–
“Kila kiongozi anapochaguliwa hana budi kujiuliza alichaguliwa kwa kura! au aliwekwa tu kwa mizengwe mizengwe.Lakini kura hizo alizipata kwa hila au kwa kufanyakazi kuonesha kuwa alifanya hivi au vile”.