Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mh. Dr. Suleiman Serera @suleiman_serera amezindua maabara ya kompyuta katika shule ya Sekondari Naisinyai wilayani Simanjiro
Shirika la Tedi Tanzania @teditanzania lenye mradi wa kuboresha elimu kupitia matumizi ya Tehama kwenye mifumo ya elimu nchini kupitia kampeni yao ya “One Computer Lab One School” wametoa kompyuta hizo na kuanza kutoa mafunzo kwa wanafunzi na walimu ili kuwapa uwezo wa matumizi ya maudhui ya masomo ndani ya kompyuta hizi.
“Kupitia maabara hii ya Kompyuta Wanafunzi wa Shule ya Naisinyai watapata mafunzo ya Masuala ya Kidigitali, Matumizi ya Kompyuta, masomo mbalimbali ya mtaala wa elimu, notes za masomo,vitabu mbalimbali, ujuzi juu ya fursa zinazopatikana katika TEHAMA na ujuzi wa elimu ya masuala ya uongozi ili kuwaandaa na soko la ajira na ushindani wa biashara duniani. Alisema Mkuu huyo wa wilaya ya Simanjiro.
Naye Gloria Anderson @glory__anderson Mkurugenzi TEDI Tanzania ametoa Shukrani kwa Serikali ya Marekani @statedept @usembassytz na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro kwa ushirikiano mkubwa waliowaonyesha katika kufanikisha mradi huo kwa kukusanya rasilimali kuanzia ngazi ya wilaya, kata na kijiji cha Naisinyai
Vile vile ameyashukuru mashirika walioshirikiana katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo katika kuandaa maudhui ya masomo mbalimbali katika kompyuta hizi ambao ni @camaraeducationtanzania @Amaizingyoullc.