Imebainika beki wa Manchester United, Harry Maguire alipewa vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana wakimwambia wanampa saa 72 ajiondoe klabuni hapo au asubiri kifo kwa kulipuliwa na bomu
Ujumbe huo ulitumwa kwake kwa njia ya barua pepe wakati akiwa mazoezini Aprili 20, 2022 baada ya United kufungwa 4-0 na Liverpool. Walimwambia wametegesha mabomu matatu nyumbani kwake na kumtaka afanye vile walivyomuagiza
Polisi walifika na mbwa wanaonusa mabomu nyumbani kwa mchezaji huyo kufanya uchunguzia lakini hawakupata chochote. Mchumba wa beki huyo, Fern Hawkins na mabinti zao wawili walihama kwa muda kwenda sehemu salama na ulinzi umeongezwa kwa Familia ya Maguire.