Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Colombia na kiungo wa zamani wa Real Madrid Freddy Rincon amefariki dunia kufuatia ajali ya gari aliyoipata Jumatatu iliyopita.
Rincon (55) alipata mafanikio makubwa katika soka Kitaifa na Kimataifa ikiwemo kucheza katika kikosi cha nchi yake kwenye Kombe la Dunia 1990,1994 na 1998.
ADVERTISEMENT
Amewahi pia kuchezea klabu mbalimbali katika nchi tofauti zikiwemo Hispania, Italia na Brazil.
ADVERTISEMENT
FIFA imetuma salamu za rambirambi kwa familia, kwa shirikisho la soka nchini Colombia, wachezaji wenzake wa zamani na wapenda soka wote duniani.