ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Kagera Tadei Mayunga amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Shelui, Igunga.
–
Meneja Uhusiano wa MSD, Etty Kusiluka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema bado wanasubiri taarifa rasmi kutoka jeshi la Polisi.
–
Ajali hiyo imetokea jana Jumanne Aprili 26, 2022 majira ya saa tisa alasiri ambapo dereva wa gari hilo anadaiwa kuwa na hali mbaya.
–
“Taarifa ni za kweli na meneja wetu amefariki tunasubiri taarifa za polisi kuhusu suala hili pamoja na chanzo cha ajali,” amesema Etty.
–
Taarifa zimeeleza kuwa meneja huyo pamoja na mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika wamefariki dunia. Meneja huyo alikuwa akitokea Bagamoyo kwenye mkutano wa mameneja wa taasisi hiyo.