ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

MIILI TISA YA WALIOFARIKI AJALI YA NJOMBE YAAGWA

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
Apr 27, 2022
in HABARI
0
MIILI TISA YA WALIOFARIKI AJALI YA NJOMBE YAAGWA
0
SHARES
229
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

 

RelatedPosts

MORGAN HERITAGE KUACHIA ALBUM YAO APRILI 21

MORGAN HERITAGE KUACHIA ALBUM YAO APRILI 21

Mar 24, 2023

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Ijumaa Machi 24,2023

Mar 24, 2023

MESUT ÖZIL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

Mar 23, 2023
Load More

Miili tisa ya waumini wa Kanisa Katoliki mkoani Njombe waliofariki kwa ajali ya gari iliyotokea Kijiji cha Igima wilayani Wanging’ombe Aprili 24, 2022 imeagwa katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki la Njombe.

–

Akizungumza wakati wa ibada ya kuaga miili hiyo jana Jumanne Aprili 26, 2022, Mkuu wa Mawasiliano wa Jimbo hilo, Padri Eusebius Kyando amesema Umoja wa Vijana Katoliki Jimbo la Njombe (Uvikanjo) pamoja na walezi wao walipata ajali wakiwa wanarudi katika safari yao ya kitume walikokwenda kuwatembelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Dorothea Upendo kilichopo Ibumila Parokia ya Mtwango.

–

ADVERTISEMENT

Amesema katika ajali hiyo, watu watatu walifariki papo hapo na wengine sita walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu hospitalini. Amesema toka mwaka 2020 Uvikanjo Parokia ya Njombe wamekuwa wakifanya kazi ya utume kwa kutembelea jumuiya ndogondogo na watu wenye mazingira magumu na kufanya matendo ya huruma katika vituo hivyo.

–

“Vijana wetu walipata ajali na wengine kufariki wakiwa katika harakati za kitume yaani kueneza injili kwa njia ya matendo mema” amesema Padri Kyando.

Amesema utume huo umewafanya vijana wengi kuimarika katika imani na hofu ya Mungu hasa katika kumpenda Mungu kupitia wahitaji.

–

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba amesema baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo alivielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kufika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe na ya Halmashauri ya mji Njombe kwa ajili ya kuangalia majeruhi pamoja na marehemu wa ajali hiyo.

–

Amesema baada ya kutoka hospitalini akiwa na kamati ya ulinzi ya Mkoa walienda katika eneo ambalo ajali hiyo ilitokea ili kujionea hali halisi. Amewataka waumini na wananchi wa Mkoa wa Njombe kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

–

“Kama neno la Mungu linavyosema shukuruni kwa kila jambo kwani hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu” amesema Kindamba.

–

Amesema Serikali ya Mkoa wa Njombe kama ilivyo kwa kanisa nayo inahitaji nguvu ya vijana kuweza kutekeleza majukumu ya taifa hivyo pigo hilo si la kanisa pekee bali hata kwa Serikali.

–

“Sisi tuliobaki tujiulize tutaondoka kwa mtindo upi ni vizuri tukajiandaa kwa kunyoosha matendo yetu na tabia zetu ili tutakapoondoka tuondoke vizuri maana kifo ni mawaidha” amesema Kindamba.

–

ADVERTISEMENT

Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbinga anayesimamia Jimbo la Njombe, Askofu John Ndimbo ameishukuru Serikali ya Mkoa huo kwa kushiriki kwa ukaribu tangu tukio hilo litokee.

–

“Narudia tena kulishukuru Jeshi letu la Polisi kwa kuitika mara moja baada ya kusikia ajali na kufika kutoa miili ya marehemu na majeruhi wetu” alisema askofu Ndimbo.

–

Baadhi ya waumini walioshiriki ibada hiyo wamesema msiba huo umewagusa kwa kiasi kikubwa na kuwaumiza kwani ni tukio kubwa kutokea hivi karibuni mkoani hapa. Wametoa wito kwa madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani

Related

ADVERTISEMENT
Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Related Posts

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Ijumaa Machi 24,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
HABARI

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA
HABARI

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI
HABARI

ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati
HABARI

NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati

by I am Krantz
Mar 23, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Alhamisi Machi 23,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In