
Mo Salah anakuwa mchezaji wa pili katika historia ya EPL kufunga na kutoa usaidizi wa goli dhidi ya Manchester United wakiwa nyumbani na ugeni rekodi iliyowekwa na Mesut Ozil miaka saba iliyopita wakati anakipiga ndani ya The Gunners (Arsenal).
Tukumbuke pia kabla ya mchezo dhidi ya Manchester United Salah alicheza michezo sita mfululizo ya EPL bila kufunga bao hata moja, gari imekuja kuwaka kwa Manchester United.
Vipi,inafaa tukisema United wamekuwa vibonde wa ligi?