MWANAFUNZI AKAMATWA KWA KUCHEZA MUZIKI MAKABURINI – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, May 19, 2022
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

MWANAFUNZI AKAMATWA KWA KUCHEZA MUZIKI MAKABURINI

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
Apr 23, 2022
in HABARI
0
MWANAFUNZI AKAMATWA KWA KUCHEZA MUZIKI MAKABURINI
0
SHARES
93
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Wizara ya mambo ya nje ya Zambia, imethibitisha kuwa mwanafunzi wa Zambia anayesoma nchini Urusi amekamatwa Jumapili iliyopita kwa kucheza muziki kwenye makaburi ya kumbukumbu ya vita ya pili ya dunia yaliyopo kwenye mji wa Khanty-Mansiysk.

RelatedPosts

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

May 19, 2022

NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

May 19, 2022

NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

May 19, 2022
Load More

Mwanafunzi huyo, Tionge Ziba mwenye umri wa miaka 21 anasoma mwaka wa kwanza kwenye chuo kikuu cha Yugra State University kilichopo kwenye mji huo.

Kwa mujibu wa Wizara hiyo, Ziba ameachiwa kwa dhamana lakini mashtaka dhidi yake yamekidhi vigezo vya kufikishwa kwa mwendesha mashtaka wa mji huo.
Taarifa za mashtaka yake zinasema kuwa video ya msichana huyo akicheza muziki kwenye makaburi hayo ilirekodiwa mnamo Aprili 14.


Mwanafunzi huyo anadaiwa kuishirikisha video hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram na kuandika maelezo ya video yakisema “nikitingisha…..kwa ajili ya marehemu [hawa], hakika wanalala unono usiku wa leo” maelezo ambayo kwa mujibu wa nyaraka za mahakama ni “maelezo ya kuudhi wanayodhaniwa yanadhihaki sera ya Nazi”.

Idara ya upelelezi ya jiji hilo tayari imeachia video ya Ziba akiomba radhi kwa kitendo hicho ingawa wakati video hiyo ilipokuwa inawekwa mtandaoni haikuwa imemtaja kwa jina wala utaifa wake.

ADVERTISEMENT

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Zambia shauri dhidi ya Ziba litachunguzwa kwa miezi mitatu na linatarajiwa kutoingiliana na ratiba zake za masomo.

Gazeti binafsi la Kommersant la nchini humo limesema huenda Ziba akakabiliwa na hukumu ya kulipa fidia ya kati ya $25,000 na $65,000 (TZS 60m – TZS 150m) au kufanya kazi ngumu kwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja hadi mitano huku kukiwa na uwezekano wa kifungo cha gerezani cha hadi miaka mitano.

Related

ADVERTISEMENT
Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Shabani Rapwi (Kijana Mchapa Kazi) WhatsApp; 0689232546 Email ;shabanimohamed932@gmail.com

Related Posts

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA
BIASHARA

WATANZANIA TAYARI KULIPIA BIMA YA AFYA

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU
HABARI

NMB FOUNDATION YATANGAZA UFADHILI SEKONDARI KIDATO CHA TANO , SITA NA ELIMU YA JUU

by I am Krantz
May 19, 2022
“PANYA ROAD” KAENI CHONJO SERIKALI IPO KAZINI
HABARI

“PANYA ROAD” KAENI CHONJO SERIKALI IPO KAZINI

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
RAIS SAMIA AMETOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU-MAJALIWA
HABARI

RAIS SAMIA AMETOA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU-MAJALIWA

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO
BIASHARA

WATEJA WA HALOTEL KUJIPATIA ZAWADI KUPITIA MATUMIZI YA MTANDAO

by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
TUMEUMIZWA NA MATOKEO YA JANA – AHMED ALLY
HABARI

TUMEUMIZWA NA MATOKEO YA JANA – AHMED ALLY

by Shabani Rapwi
May 19, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In