Jeshi la Polisi nchini Kenya limethibitisha kutokea kwa mauaji ya Mwanariadha wa kike kutoka nchini humo
Damaris Muthee Mutua (28) ambapo mauaji hayo yametokea huko Iten mji wa Kenya ambapo mwanariadha wa Olimpiki Agnes Tirop, aliuawa miezi sita iliyopita.
Damaris alizaliwa nchini Kenya lakini alikuwa na uraia wa Bahrain, Maafisa wanasema aliuuawa kwa kudungwa kisu na Wanamsaka mpenzi wake, mwanariadha wa Ethiopia ambaye polisi wanasema ni mshukiwa mkuu.
Iten ni kambi ya mafunzo kwa wakimbiaji wa masafa marefu na Mwezi Oktoba mwaka jana mauaji ya mwanariadha Agnes Tirop yaliyoleta taharuki huko Kenya na Mumewe bado yuko kizuizini na anakanusha kuhusika na mauaji hayo.