Nyota wa mtandao TikTok kutoka Misri, Haneem Hossam amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani.
Hukumu hiyo inakuja baada ya mahakama ya kumkuta na hatia ya usafirishaji haramu wa binadamu.
Haneen Hossam alishtakiwa kwa kutengeneza pesa kwa njia ya kuwarubuni wasichana kupitia mtandao huo wa kushirikishana picha za video.
Haneem alikataa mashtaka hayo ambayo yanahusishwa na video yake ya kuwaalika wafuasi wake kwenye mtandao huo kusambaza video za mubashara na kupata malipo kwa kufanya hivyo. Wanaharakati wa haki za binadamu Haneem amehukumiwa kwa hila na ni sehemu ya kuwadhibiti wahamasishaji wanawake kwneye mitandao ya kijamii.
Haneen alifanikiwa kupata zaidi ya wafuasi 900,000 kwa kuigiza kuimba nyimbo na kushirikisha watu kwenye mtandao wa TikTok. Alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2020 baada ya kuwaalika wafuasi wake wanawake kwenye mtandao mwingine wa kushirikisha video wa Likee alikowaambia watapata pesa kwa kushirikisha watu video zao.
Mahakama ya Uchumi ya Misri ilimkuta na hatia sambamba na nyota mwingine wa TikTok, Mawada al-Adham kwa makosa ya kukiuka tunu na misingi ya familia” na wakahukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani na kulipishwa faini ya paundi za Misri 300,000 (TZS 49m).
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT