Kocha wa muda wa Machester United, Ralf Rangnick amesema huwenda kiungo wao Paul Pogba (29), ukawa ndio msimu wake wa mwisho kuichezea timu hiyo kutokana na jeraha alilolipata, lakini pia mkataba wake unatarajia kumalizika mwezi wa sita mwaka huu.
Kiungo huyo anatarajiwa kuwa nje kwa wiki nne kutoka na majeraha ya mguu aliyopata na kushindwa kuendelea na mchezo dhidi ya Liverpool.