ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Rais Samia Suluhu kuzindua kitabu cha historia ya muungano

I am Krantz by I am Krantz
Apr 21, 2022
in HABARI
0
Rais Samia Suluhu kuzindua kitabu cha historia ya muungano
0
SHARES
129
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kuzindua kitabu cha Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa lengo la kuelimisha umma. Kitabu hicho kitazinduliwa tarehe 26 Aprili, 2022 siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya uzinduzi, Ofisi imepanga kuwa na mpango endelevu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu historia ya Muungano na masuala ya msingi kuhusu Muungano. Inatarajiwa kuwa, Mpango wa elimu kwa umma utaongeza uelewa wa historia ya Muungano na masuala mengine muhimu kuhusu Muungano.

RelatedPosts

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

Aug 9, 2022

Uber yasitisha huduma zake Tanzania, yazitaja nauli elekezi Latra kama sababu.

Apr 14, 2022

Mbunge Shabiby atoa Mwarobaini Kupanda bei mafuta

Apr 7, 2022
Load More

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameyasema hayo leo 20/04/2022 wakati wa Mkutano na waandishi wa habari akiambatana na Mawaziri wenzake wawili ambao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) – Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma

Dkt. Jafo alisema, Muungano unapotimiza miaka 58 ni jambo la kujivunia na hatuna budi kuendeleza mazuri yaliyopatikana kutokana na Muungano na kusisitiza kuwa maadhimisho ya Muungano kwa mwaka huu yataambatana na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu historia ya Muungano, tulipotoka, tulipo na tunapoelekea kupitia kongamono litakaloongozwa na wabobezi mahiri wa masuala ya Muungano ambao wataeleza kwa kina historia ya Muungano, Misingi ya Muungano na Mafanikio ya Muungano kutoka pande zote mbili za Muungano.

“Wananchi wa pande zote za Muungano wamezaliwa baada ya Muungano, hali inayoonesha wazi uwepo wa umuhimu wa utoaji wa elimu ya historia ya Muungano pamoja na masuala ya msingi yanayohusu Muungano” Jafo alisisitiza.

ADVERTISEMENT

Aidha, Waziri Jafo amesema kuwa kwa lengo lilelile la kuelimisha umma hasa vijana, yameandaliwa mashindano ya Insha kuhusu Muungano kwa wanafunzi wa shule za Sekondari ambapo kutakuwa na washindi sita (3 kutoka Tanzania Bara na 3 kutoka Tanzania Zanzibar) ambao watapewa zawadi siku ya tarehe 26 Aprili, 2022. Insha hizo zinawapa fursa wanafunzi kuelezea historia ya Muungano; mafanikio na changamoto za Muungano; na nafasi ya vijana katika kulinda na kudumisha Muungano.

Kwa upande wake Waziri Simbachawene amesema Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho na Sherehe Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameridhia kuwa Mikoa, Taasisi za Serikali na Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama viadhimishe Maadhimisho hayo kwa kufanya shughuli za Kijamii katika maeneo yao ya karibu au Vikosi na Kambi zao kama vile kufanya usafi, kupanda Miti na kutoa huduma za afya. Kitendo hiki adhimu kitaleta hamasa kubwa, Umoja na mshikamano na kuuenzi Muungano wetu kwa heshima na taadhima kubwa.

ADVERTISEMENT

Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Waziri Juma amesema maadhimisho ya mwaka huu yanaenda sambamba na Maonesho ya Taasisi za Muungano yatakayoanza tarehe 22 Aprili 2022 mpaka tarehe 06 Mei 2022 pamoja na Kongamano litakaloenda sambamba na kumbukizi ya Miaka 50 ya Muuasisi wa Muungano Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Related

Tags: SAMIATANZANIA
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
HABARI

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA
HABARI

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI
HABARI

ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati
HABARI

NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati

by I am Krantz
Mar 23, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Alhamisi Machi 23,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
YANGA PRINCESS, SIMBA QUEENS HAKUNA MBABE
HABARI

YANGA PRINCESS, SIMBA QUEENS HAKUNA MBABE

by Shabani Rapwi
Mar 22, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
April 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930  
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In