Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martin Shigella amenunua picha ya kuchorwa ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa thamani ya shilingi Milioni moja kutoka kwa mchoraji Mboya Hosiana mkazi wa Gairo mkoani Morogoro.
ADVERTISEMENT
Aidha Shigella amesema kuwa ni wakati wa watanzania wote kumuunga mkono Rais Samia ili kumtia moyo katika kampeni yake ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini. Mchoro huo unaonesha picha ya Rais Samia, Royal Tour pamoja na baadhi ya picha za vivutio vya utalii.
ADVERTISEMENT