Kikosi cha nyota 22 wa Ruvu Shooting kimeanza safari ya kuelekea Kigoma tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Mei 4 dhidi ya Yanga.
–
Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa mchezo huo waliouhamishia kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kwa mujibu wa kanuni.
–
Katika msafara huo Kocha Boniface Mkwassa amewaacha wachezaji watatu, Elius Maguri, Hamad Majimengi na Paul Ngarema kwa sababu mbali mbali.
–
“Hawa watatu hatukusafiri nao, wengine ni majeruhi na wengine wana sababu binafsi.
Mbali ya hao, wachezajii wengine 22 wako vizuri na tayari kea mechi yetu ya Mei 4,” amesema Mkwasa.