ADVERTISEMENT
Timu ya Taifa ya Wanawake U17, Serengeti Girls wapo tayari kukabiliana na Burundi katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia hapo kesho, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
–
Mkurugenzi wa Mashindano TFF, Salum Madadi amesema japo mtanange huo ni muhimu kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kwenda Kombe la Dunia na kusema kuwa vijana wamejiandaa kikamilifu kuwakabili Burundi.
–
Kwa upande wake mchambuzi wa michezo, Clement John amesema kuwa Serengeti Girls wapo kwenye nafasi nzuri ya kupata ushindi kwenye mechi hiyo hapo kesho ili kujihakikishia nafasi ya kucheza na Cameroon ama Zambia mwishoni mwa mwezi Mei.
Chanzo – TBC
ADVERTISEMENT