Serikali imesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 inatarajia kuajiri watumishi wa sekta ya Afya 7612 ambao watapelekwa katika Halmashauri zote Nchini
Hayo yamesemwa leo April, 20,2022 na Naibu waziri wa Tamisemi anayeshughulikia masuala ya Afya Dkt. Festo John Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Malaam Mhe. Josephine Genzabuke lililohoji Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la ukosefu wa Watumishi wa Kada mbalimbali katika Hospitali nchini pamoja na ukosefu wa Vifaa Tiba.
Aidha Mhe. Dkt. Dugange amesema Serikali imetenga Bilioni 69.95 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwa Zahanati,vituo vya Afya na Hospitali za Halmashauri zilizokamilika