Klabu ya Simba SC imeomba ulinzi wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Afrika Kusini wakiwa safarini na wakifika nchini Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano Shirikisho barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa April 24, 2022.
Klabu hiyo imeeleza kuwa, vitisho visivyo vya moja kwa moja vilivyotolewa na kocha wa Orlando Pirates havipaswi kupuuzwa ndio maana wanaomba ulinzi katika kipindi chote klabu hiyo itakapokuwa nchini Afrika Kusini. Pia Simba imeeleza inapeleka malalamiko CAF na kwa balozi zote mbili yaani Tanzania na Afrika Kusini kuhusu shutuma walizopewa na kocha wa Orlando.