Klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Orlando Pirates kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika kwa sare ya 0-0 huku timu zote mbili zikishambuliana kwa zamu.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikifanya mashambuli ya kutafuta bao na mnano wa dakika ya 67 Simba wakaandika bao kupitia kwa beki Shomari Kapombe dakika ya 67′ kwa mkwaju wa penati baada ya kufanyika mchezaji wa Orlando kufanya madhambi kwenye eneo la Box na mwamuzi kuruhusu penati.
Mchezo wa pili wa marudiano wa robo fainali utapigwa April 24, 2022 kwenye uwanja wa Orlando huko Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.