Shirika la umeme nchini (TANESCO) limesema limekamilisha matayarisho ya kuiandaa transfoma yenye uwezo wa MVA 30 ambayo imesafirishwa rasmi kuelekea kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Msamvu Mkoani Morogoro.
Transfoma hiyo itasaidia kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwa Wakazi wa Mkoa wa Morogoro na baadhi ya maeneo jirani ikiwemo mkoa wa Tanga ambao kwa sasa unapata changamoto ya upungufu wa umeme.