Shirika la viwango nchini Tanzania limewakumbusha wazalishaji wa matofali kuwa TBS ndiyo wenye jukumu la kuweka na kusimamia viwango vya kitaifa hivyo kuhakikisha wanafuata matakwa ya Kiwango wakati wa uzalishaji wa bidhaa hiyo.
ADVERTISEMENT
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya TBS na Wazalishaji wa matofali, Kaimu mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandisi Johaness Maganga amesema kuwa TBS inajukumu la kutoa mafunzo na ushauri viwandani juu ya uzalishaji wa bidhaa bora.
Aidha amesema kuwa jukumu lingine pia ni kupima na kuhakiki vipimo vinavyotumika viwandani pamoja na kuelimisha umma juu ya masuala yote yanayohusu uwekezaji na usimamizi wa viwango pamoja na udhibiti wa ubora wa bidhaa.

Katika hatua nyingine Mhandisi Maganga amesema kuwa Tbs itaendelea kuandaa mikutano mbalimbali kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchni lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango. Mhandisi Maganga amewaasa wazalishaji wa matofali waliohudhuria mkutano kutumia fursa hiyo kujifunza.
ADVERTISEMENT