Ameandika, Kiungo wa zamani wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC na Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Amri Kiemba.
Sio dhambi Simba kushinda mechi za nyumbani pekee kwenye michuano ya Africa kutokana na mifumo ya usimamizi wa mchezo wenyewe kutoa faida zaidi kwa mwenyeji ndio maana mgeni akapewa faida ya goli la ugenini.
Imewachukua UEFA miaka mingi kurekebisha usimamizi wa michezo yao na kujiridhisha kunakuwepo na usawa wa ushindani ndani ya kiwanja kwa asilimia kubwa ndipo umeona wameondoa faida ya goli la ugenini
Kwa wale ambao hawajawahi kushiriki michuano ya Africa ni rahisi kushambulia mikakati ya timu kujipanga kiakili kuhakikisha mechi za nyumbani yanapatikana matokeo chanya na kuisaidia timu kuendelea mbele kwenye michuano husika. Michuano ya Africa ni tofauti na mnavyoijadili vijiweni inahitaji kuwa na timu imara ndani ya kiwanja lakini pia timu bora na bobezi kupambana nje ya uwanja kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa timu kushindana na kupata matokeo kwani ndio utaratibu wa michuano ili kama timu inafungwa basi mjadala uwe ni kuboresha kikosi na sio tumehujumiwa
Kama utaamini kwamba benchi la ufundi linatosha kuiandaa timu kushindana ndani ya kiwanja inatosha kwenye michuano ya Africa utaendelea kufukuza waalimu na kufanya usajili kila msimu hivyo basi bila kupepesa kama unataka kushindana Africa inakupasa kushindana kwa namna wanavyoshindana tengeneza timu bora ndani ya uwanja na timu bora nje ya uwanja
Kwa hili niwapongeze Simba kwa kuanza kushindana namna ambavyo tulipaswa kushindana toka awali ndio maana kutokana na ukomavu huo hatusikii tena wakilalamika juu ya hujuma kwenye michuano
Hizi propaganda zinazoendelea ni khofu ya timu pinzani ya kucheza na Simba kwa mkapa kwani wanajua ugumu wa kupata matokeo uwanjani hapo na baadhi ya watanzania wamelibeba kama agender kuhakikisha wageni wanacheza kama wako nyumbani na sio ugenini inafikirisha.
Wakati mwingine badala ya kutaka watu wote waliokuzunguka wasiwenacho kama wewe unapaswa kufikiria ni nani utamuomba msaada ukikwama kwa maana hiyo tunapaswa kujivunia mafanikio ya Simba kama nchi kwani sasa hivi tunaanza kuzoea kupeleka timu nne .MKila la kheri Simba, kila la kheri Tanzania